AJALI ILIOTOKEA FORT TENAN, 55 WAFARIKI

 Mwendo wa saa kumi asubuhi eneo la fort tenan kaunti ya kericho biwi la simanzi lilitanda pale ambapo  basi la kampuni ya Home boyz lenye nambari za usajili KBX 092J linalo milikiwa na bwanyenye mmoja kutoka mjini Kakamega limefanya ajali iliofuatia watu hamsini kupoteza maisha yao na wengine zaidi ya kumi na tano kupata majeraha si haba. vile vile basi hilo lilikua limebeba abiria kupita kiasi chake.


      Takriban masaa tano baadae hamna ambulenzi ya hosipitali yeyote  iliyokua imefika kusaidia str65manusura. kulingana na manusura mmoja dereva huyo aliekuwa jeuri kupitiliza na hata kuwapuuza  wasafiri walipo mwambia dereva apunguze  mwendo ila kw kutia ntaa masikioni.

      Licha ya hayo kampuni hiyo ya mabasi ya Homeboyz haikua  na leseni ya kufanya kazi usiku hii ni kwa mujibu wa kamanda wa trafiki wa kaunti ya kericho.

      Kulingana wakaazi wa Fly over, Fort tenan  wamesema kwamba dereva alijaribu kupita lori na hapo ndipo gari lilipoteza mwelekeo na kubingirika mara kadhaa, hata hivyo eneo hilo limesemekana  kushuhudia zaidi ya ajali tano chini ya muda wa wa miaka mbili. majeruhi saba wamepelekwa katika hosipitali ya muhoroni na wengine wanane wanahudumiwa katika hosipitali ya fort tenan.

      Ikumbukwe hii ndio ajali ya pili kwa ukubwa iliyo husisha gari moja.  mabaki ya basi hilo yamekokotwa kuelekea kituo cha polisi. hata hivyo wamiliki wa basi hilo washakamatwa

         Mola awalaze wote waliofariki pahali pema peponi


                             by hassan iddris




Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog